Wananchi wa Halmashauri ya Wilaya ya Babati wameendelea kuishukuru serikali kwa kutoa kiasi cha Tsh 1,000,000,000 ( Billion Moja kwa ajili ya ujenzi wa jengo la Utawala , Makuu Makao Makuu ya halmashauri ya Wilaya ya Babati ambalo limefika hatua nzuri ya utekelezaji .Hayo yamesemwa na Diwani wa Kata ya Arri Mhe. Paul Masong alipotembelea eneo la mradi inakojengwa halmashauri hiyo kijiji cha Endasago kata ya Arri. "Ninapokuja hapa mara kwa mara nafurahishwa na ujenzi wa jengo hilo ujenzi unaenda kwa kasi sana,lakini nawakilisha wananchi wangu wanapongeza serikali kwa kuleta mradi mkubwa katika kata yangu" amesisitiza kiongozi huyo. Kiongozi huyo ameomba serikali kuendelea kutoa fedha kwa ajili ya kukamilisha mradi huo unaojengwa na shirika la SUMA JKT . ili mradi huo uweze kukamilika kwa wakati na kutoa huduma kwa wananchi.
Halmashauri ya wilaya ya Babati
Anwani: P.O BOX 400, Babati.
Simu ya mezani: Simu Na. 027-2531011
Simu ya Kiganjani: 0620444641,075486577
Barua pepe: info@babatidc.go.tz,ded@babatidc.go.tz
Copyright ©2020 Babati District Council . All rights reserved.