Baraza la Madiwani la Halmashauri ya Wilaya ya Babati limepongeza Timu ya Menejiment ikiongozwa na Mkurugenzi Mtendaji Anna Mbogo kwa usimamizi wa miradi endelevu ya usafi na mazingira( SRWSS) kwa kipindi cha miaka 5 kuanzia mwaka 2021 hadi 2026. Haya yamesemwa na Mwenyekiti wa Baraza hilo leo Mhe. John Noya kwenye mkutano wa Baraza la Madiwani lililofanyika katika Ukumbi wa Halmashauri. " Tunawapongeza Sana Timu ya menejiment kwa utekelezaji mradi ambayo imeleta manufaa katika maeneo yetu vijijini" amesisitiza kiongozi huyo.Mhe Noya amesema mradi huo ulitekelezwa wa kwa utaratibu wa lipa Kwa matokeo (EP4R) ambapo Halmashauri imeweza kupata Tsh 2.7 Bilioni na kutekeleza miradi mbalimbali. . Miradi iliyotekelezwa kupitia mradi wa usafi wa mazingira ni pamoja ujenzi wa vinawia mikono Zahanati,Madarasa Vyoo katika Zahanati na shule za Msingi, na miundombinu ya maji
Halmashauri ya wilaya ya Babati
Anwani: P.O BOX 400, Babati.
Simu ya mezani: Simu Na. 027-2531011
Simu ya Kiganjani: 0620444641,075486577
Barua pepe: info@babatidc.go.tz,ded@babatidc.go.tz
Copyright ©2020 Babati District Council . All rights reserved.