Wanufaika wa mradi wa kunusuru kaya Masikini( TASAF) H/Wilaya ya Babati wameishukuru serikali kwa kuendelee kutoa fedha kwa walengwa wa mradi huo. Akizungumza Bi Juliana Tlatla mkazi wa kijiji cha Kwaraa kata ya Endakiso kwa niaba ya walengwa ktk kijiji hicho(waliofika kupokea fedha) amesema wanaishukuru serikali kuendelea kutoa fedha kwa lengwa ili ziwasaidie katika kujikwamua na umasikini.
Bi Juliana amewaomba wanufaika wenzake kutumia fedha hizo kuanzisha miradi ya maendeleo mfano ufugaji, kilimo cha mbogamboga ,biasharakama yeye anavyofanya ili kujiongezea kipato. Naye mratibu wa TASAF H/Wilaya ya Babati Ndg Regina Mlinga amesema kwa kipindi cha Julai hadi August 2022 serikali kuu imetoa fedha kiasi cha Tsh 516,225,750 kwa ajili ya mradi wa kunusuru kaya Masikini ambapo walengwa 14,475 katika vijiji vyote 102 vya H/Wilaya ya Babati watanufaika na fedha hizo.Mratibu huyo amesisitiza walengwa kutumia fedha hizo vizuri ikiwa ni pamoja na kuanzisha shughuli za ujasiliariamali ambazo zitawaongezea kipato.
Halmashauri ya wilaya ya Babati
Anwani: P.O BOX 400, Babati.
Simu ya mezani: Simu Na. 027-2531011
Simu ya Kiganjani: 0620444641,075486577
Barua pepe: info@babatidc.go.tz,ded@babatidc.go.tz
Copyright ©2020 Babati District Council . All rights reserved.