Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Babati Mhe. Nicodemus Tarmo amewashukuru wananchi, Viongozi na Watumishi kutoka ndani ya kata na nje ya kata ya Madunga kwa kuchangia kiasi cha Tsh milioni Ishirini na sita ( 26,000,000) Kwa ajili ya kukamilisha ujenzi wa Zahanati ya Kijiji cha Gidngwar katika kata ya Madunga. Mhe. Tarmo amesema hayo Léo akiwa Mgeni Rasmi kwenye Harambee iliyoitishwa na Diwani wa Kata ya Madunga Mhe. John Noya na kufanyika ofisi ya Kijiji cha Gidngwar "Nawashukuru Viongozi na wananchi wote wa kata ya Madunga na nje ya Madunga kuanzia ngazi ya kitongoji kwa kuchangia vifaa, mazao, mifugo, na fedha taslimu vyote vikiwa na thamani ya Million 26".amesisitiza Kiongozi huyo.Akitoa neno lá shukurani Diwani wa Kata hiyo Mhe. John Noya ambaye ni Makamu Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Babati amesema kukamilika kwa Zahanati hiyo kutakuwa mkobozi kwa wananchi wa Kijiji hicho kwani hutembea Km 4 hadi km 6 kufuata huduma za Afya katika Zahanati za vijiji na kata jirani na kuhaidi kusimamia fedha zote zilizochangwa kufanya kazi iliyokusudiwa. Harambee hiyo ni ya pili kwa utaratibu aliyojiwekea Diwani huyo ambapo mwaka 2017 alihitisha harambee ya ujenzi wa Zahanati ya kijiji chá Madunga na kupata kiasi cha Tsh 18,000,000 na Zahanati hiyo Kwa sasa inatoa huduma Kwa wananchi wa Kijiji cha Madunga kata ya Madunga.
Halmashauri ya wilaya ya Babati
Anwani: P.O BOX 400, Babati.
Simu ya mezani: Simu Na. 027-2531011
Simu ya Kiganjani: 0620444641,075486577
Barua pepe: info@babatidc.go.tz,ded@babatidc.go.tz
Copyright ©2020 Babati District Council . All rights reserved.