Wananchi wa kata ya Nar katika Halmashauri ya Wilaya ya Babati wemepaza sauti za shukurani kwa Rais Mhe. Dkt Samia Suluhu Hassan kwa kuwapatia fedha kiasi cha Tshs 89,400,000 kwa ajili ya ujenzi wa vyumba 3' vya madarasa na Matundu 8 ya vyoo katika shule ya sekondari Nar. Wananchi hao wamepaza sauti leo mbele ya Kamati ya Fedha, Mipango na Uongozi ya H/ Wilaya wakati kamati hiyo ikifuatilia na kukagua miradi ya maendeleo kwenye kata." Sisi wananchi wa kata ya Nar Tunamshukuru Mhe . Rais kwa kutupatia fedha kujenga vyumba vya madarasa na vyoo Mungu ambariki" wananchi wamesikika wakisema . Naye Makamu m/Kiti wa H/ Wilaya ya Babati Mhe. Yahaya Loya amewapongeza wananchi hao kwa usimamizi na ujenzi wa viwango madarasa na vyoo na kusisitiza mradi huo ukamilike kwa wakati na uanze kutoa huduma.Madarasa hayo yamefika hatua ya kuanza upauzi..
Halmashauri ya wilaya ya Babati
Anwani: P.O BOX 400, Babati.
Simu ya mezani: Simu Na. 027-2531011
Simu ya Kiganjani: 0620444641,075486577
Barua pepe: info@babatidc.go.tz,ded@babatidc.go.tz
Copyright ©2020 Babati District Council . All rights reserved.