Wananchi wametakiwa kutoa taarifa sahihi za waalifu wanaofanya vitendo vya ukatili wa kijinsia kwa uongozi ulio karibu nao ili waweze kukamatwa mara moja.Hayo yamesemwa leo na Mkuu wa Wilaya ya Babati Mhe Lazaro Twange kwenye mkutano wa hadhara wa kusikiliza na kutatua kero za wananchi uliofanyika uwanja wa Mpira katika kijiji cha Magugu kata ya Magugu." Ni kweli mnastahili kukasirika kwani vitendo vya ubakaji, mauaji vimezidi kata ya Magugu hivyo toeni taarifa sahihi ili watu waovu waweze kukamatwa mara moja" amesisitiza kiongozi huyo. Mhe. Twange ameendelea kuwaomba wananchi hao kutoa taarifa sahihi kwa viongozi ili vitendo viovu vinavyofanyika viweze kumalizika.Katika mkutano huo wananchi wa kata za Magugu, Mwada, Nkait, Kisangaji na Magara wamehudhuria kwa wingi na kuuliza kero zao ambazo zimetatuliwa na uongozi wa Halmashauri , BAWASA, TARURA, RUWASA na TANROAD
Halmashauri ya wilaya ya Babati
Anwani: P.O BOX 400, Babati.
Simu ya mezani: Simu Na. 027-2531011
Simu ya Kiganjani: 0620444641,075486577
Barua pepe: info@babatidc.go.tz,ded@babatidc.go.tz
Copyright ©2020 Babati District Council . All rights reserved.