Wananchi Wilayani Babati wametakiwa kuanza kulima zao la Kahawa na Pamba ili kujipatia kipato na kukuza uchumi wa Viwanda. Hayo ameyasema Mkuu wa Wilaya ya Babati Mhe. Raymond Mushi kwenye Kikao cha Baraza la Madiwani Halmashauri ya Wilaya Babati wakati wa kuwasilisha taarifa za Serikali, Kilimo cha Kahawa na Pamba kifufuliwe aliwasisitiza Wahe. Madiwani. Aidha Mkuu wa Wilaya aliwaeleza Madiwani kuendelea kuwahamasisha wananchi kulima kwa kutumia Kontua ili kuzuia makorongo ambayo yanajitokeza kwa kasi katika Halmashauri ya Wilaya ya Babati.
Halmashauri ya wilaya ya Babati
Anwani: P.O BOX 400, Babati.
Simu ya mezani: Simu Na. 027-2531011
Simu ya Kiganjani: 0620444641,075486577
Barua pepe: info@babatidc.go.tz,ded@babatidc.go.tz
Copyright ©2020 Babati District Council . All rights reserved.