Mkuu wa Mkoa wa Manyara Mhe. Makongoro Nyerere amewataka Wananchi wa Mkoa wa Manyara kuwapeleka Shule watoto wote wenye umri wa kwenda Shule bila kikwazo chochote . Hayo ameyasema leo Kwa nyakati tofauti wakati akitembelea kukagua miundombinu ya Shule Kwa ajili ya mapokezi ya kidato Cha kwanza 2023 na ukaguzi wa Barabara ya Magugu Kisangaji katika Kata ya Magugu H/ Wilaya ya Babati."Mama Samia amejenga Madarasa mengi yanatosha na kubaki Wananchi wapelekeni Shule watoto wote wenye umri wa kwenda Shule na Wale waliochaguliwa kujiunga Kidato Cha kwanza nao waende Shule bila kikwazo chochote" amesisitiza kiongozi huyo . Akiwa Katika Shule ya Sekondari Magugu iliyoko Kata ya Magugu Mkuu wa Mkoa amesisitiza kuwa Wanafunzi wasirudishwe nyumbani baada ya kuwasili Shuleni Kwa madai ya kukosa Michango mbalimbali. Wanafunzi wa Kidato Cha kwanza Shule za sekondari Magugu wameshukuru Mhe. Rais Dr. Samia Suluhu Hassan kwa ujenzi wa Madarasa pamoja na viti na kuhaidi kusoma Kwa bidii na kulinda miundombinu ya Shule.
Halmashauri ya wilaya ya Babati
Anwani: P.O BOX 400, Babati.
Simu ya mezani: Simu Na. 027-2531011
Simu ya Kiganjani: 0620444641,075486577
Barua pepe: info@babatidc.go.tz,ded@babatidc.go.tz
Copyright ©2020 Babati District Council . All rights reserved.