Wajumbe wa Baraza la Madiwani Halmashauri ya Wilaya ya Babati wameshukuru Serikali kwa kutoa fedha za ujenzi wa Kituo Cha Afya Kipya cha Kiru katika kata ya Kiru Tsh 250,000,0000 , ujenzi wa Mabweni mawili Shule ya Sekondari Gidas kata ya Gidas Tsh ( 260,000,000 ) na Ujenzi wa Mabweni mawili Shule ya Sekondari Kisangaji kata ya Kisangaji Tsh 260,0000,000).Akitoa Taarifa ya Serikali leo kwenye Baraza la Madiwani, Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Babati Anna Mbogo amesema Serikali inayoongozwa na Mhe. Dkt Samia Suluhu Hassan imeleta fedha nyingi ikiwemo ujenzi wa Kituo na Mabweni tajwa hapo juu na miradi mingine mingi. Kwa Upande wake Diwani wa Kata ya Kiru Keremu B. Keremu ameshukuru Serikali kuwapatia kituo kata ya Kiru kwani ilikuwa hitaji lao kwa muda mrefu. Wakati huo Mwenyekiti wa H/ Wilaya Mhe. John Noya na Wajumbe wa Baraza hilo Wamempongeza Mbunge wa Jimbo la Babati Vijijini Mhe. Daniel Sillo kwa kazi nzuri na kuwatumikia vyema kwani ameleta miradi na Maendeleo kwa wananchi .
Halmashauri ya wilaya ya Babati
Anwani: P.O BOX 400, Babati.
Simu ya mezani: Simu Na. 027-2531011
Simu ya Kiganjani: 0620444641,075486577
Barua pepe: info@babatidc.go.tz,ded@babatidc.go.tz
Copyright ©2020 Babati District Council . All rights reserved.