Halmashauri ya Wilaya ya Babati Kwa kushirikiana na Wadau wa Maendeleo na Wananchi wa Kata za Madunga na Bashnet wamejenga ofisi za Kata kurahisisha upatikanaji wa huduma . Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Babati Anna Mbogo amesema Halmashauri ya Babati itaendelea kutenga na kutoa fedha za mapato ya ndani Kila mwaka kujenga ofisi za Kata na Vijiji ili kurahisisha utoaji wa huduma na kudumisha utawala Bora.
Madiwani wa Kata hizo Jovitha Mandoo(Kata ya Bashnet) na John Noya Kata ya Madunga) Kwa nyakati tofauti katika Kata zao wameshukuru Serikali, wadau wa Maendeleo na Wananchi kwa kukubali kuchangia fedha na vifaa kujenga ofisi za Kata ili kurahisisha utoaji wa huduma na utawala Bora katika maeneo yao.
Halmashauri ya wilaya ya Babati
Anwani: P.O BOX 400, Babati.
Simu ya mezani: Simu Na. 027-2531011
Simu ya Kiganjani: 0620444641,075486577
Barua pepe: info@babatidc.go.tz,ded@babatidc.go.tz
Copyright ©2020 Babati District Council . All rights reserved.