Wadau wa Afya wameipongeza Halmashauri ya Wilaya ya Babati kwa kupambana na magonjwa ya mlipuko na kipindupindu. Hayo yamesemwa na wadau wa Afya leo kwenye kikao cha Afya ya Msingi (PHC) kilichofanyika leo katika ukumbi wa H/ Wilaya ya Babati " Tumeridhika na hatua zinazochukuliwa na Halmashauri ya Wilaya katika kupambana na magonjwa ya mlipuko na kipindupindu usafi na Elimu ya kujikinga iendelee " wamesisitiza wadau hao . Naye mwenyekiti wa kikao hicho Mkuu wa Wilaya ya Babati Mhe. Lazaro Twange ambaye amewakilishwa na Mkurugenzi Mtendaji wa H/ Wilaya ya Babati Anna Mbogo ameagiza ya usafi wa nyumba kwa nyumba , ukaguzi, ujenzi wa vyoo na elimu ya kujikinga iendelee kutolewa ili kuhakikisha ugonjwa wa kipindupindu haunei tena . Wakati huo huo Mkurugenzi Mtendaji ameagiza tena Maofisa Elimu kata kukagua usafi wa vyoo kwa shule za msingi na sekondari kila siku asubuhi na jioni ili kuzuia magonjwa ya mlipuko na kipindupindu.
Halmashauri ya wilaya ya Babati
Anwani: P.O BOX 400, Babati.
Simu ya mezani: Simu Na. 027-2531011
Simu ya Kiganjani: 0620444641,075486577
Barua pepe: info@babatidc.go.tz,ded@babatidc.go.tz
Copyright ©2020 Babati District Council . All rights reserved.