Viongozi wapya wa serikali za Mitaa waliochaguliwa katika Halmashauri ya Wilaya ya Babati wameshukuru Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Babati Anna Mbogo kwa kuwapa mafunzo juu ya majukumu yao . Hayo yamesemwa na viongozi mbalimbali leo kwa nyakati tofauti katika kata za Mamire na Gallapo mahali mafunzo ya viongozi yalipofanyika. "Tunamshukuru Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri yetu kwa kuleta mafunzo hayo ili kufahamu majukumu na mipaka yetu " wamesisitiza. Viongozi hao wameendelea kusema kubwa katika mafunzo hayo wamepata nyenzo watakazotumia katika kuwaletea wananchi maendeleo katika vijiji vyao. Mafunzo hayo yamelenga kuwapa viongozi hao majukumu yao, mipaka yao, ushirikishaji wa wananchi kujiletea maendeleo, ulinzi na usalama, utunzaji wa mazingira, maadili, ukatili wa kijinsia na mambo mengine yatakayowawezesha katika uongozi wake. Mafunzo ya Viongozi wapya katika halmashauri ya Wilaya yatafanyika katika vijiji vyote 102 kuwapa uelewa na majukumu yao katika kuendeleza serikali.
Halmashauri ya wilaya ya Babati
Anwani: P.O BOX 400, Babati.
Simu ya mezani: Simu Na. 027-2531011
Simu ya Kiganjani: 0620444641,075486577
Barua pepe: info@babatidc.go.tz,ded@babatidc.go.tz
Copyright ©2020 Babati District Council . All rights reserved.