Halmashauri ya wilaya ya Babati leo imehitimisha mafunzo ya viongozi wapya waliochaguliwa katika uchaguzi wa serikali za mitaa tech 27/11/2024. Katika hotuba yake mara baada ya Mafunzo kwa niaba ya Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Babati Ndg Godfrey Japhari amewataka viongozi hao kwenda kutenda haki, kujituma kufanya kazi kwa bidii ili kuwaletea wananchi maendeleo. Ndg Japhari ambaye ni Mwanasheria wa H/Wilaya ya Babati amesisitiza viongozi hao kuhakikisha wanaitisha na kufanya vikao vya kisheria kwa mujibu wa ratiba. . Mafunzo hayo yaliyoanza tarehe 11/12 /2024 yamefanyika katika vituo 12 na leo yamehitimishwa katika kituo cha shule ya sekondari Mbugwe kata ya mwada
Halmashauri ya wilaya ya Babati
Anwani: P.O BOX 400, Babati.
Simu ya mezani: Simu Na. 027-2531011
Simu ya Kiganjani: 0620444641,075486577
Barua pepe: info@babatidc.go.tz,ded@babatidc.go.tz
Copyright ©2020 Babati District Council . All rights reserved.