Halmashauri ya Wilaya ya Babati imeendelea kutoa mafunzo kwa viongozi wapya waliochaguliwa kwenye uchaguzi wa serikali za mitaa tarehe 27/11/2024. Kwa niaba ya Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Babati Ndg Benedict Ntabagi ambaye ni Afisa Utumishi amewataka viongozi hao kwenda kutenda haki , kufanya kazi kwa bidii na kuhamasisha maendeleo katika maeneo yao.Kwa leo Mafunzo hayo yamefanyika katika vituo vya kata za Secheda na Bashent na takribani wajumbe 500 kutoka kata sita wamehudhuria mafunzo hayo . Kwa upande wao wajumbe wamepongeza Halmashauri ya Wilaya Babati kwa kutoa mafunzo hayo na wakaomba mafunzo hayo yawe endelevu. . Mafunzo kwa viongozi wapya yanalenga kuwapa uelewa juu ya majukumu na mipaka yao katika kuongoza wananchi
Halmashauri ya wilaya ya Babati
Anwani: P.O BOX 400, Babati.
Simu ya mezani: Simu Na. 027-2531011
Simu ya Kiganjani: 0620444641,075486577
Barua pepe: info@babatidc.go.tz,ded@babatidc.go.tz
Copyright ©2020 Babati District Council . All rights reserved.