Afisa Mwandikishaji Jimbo la Babati Vijijini Anna Mbogo amekutana na Viongozi wa vyama vya Siasa kwa ajili ya maandalizi ya Uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga kuwa Awamu ya Pili na uwekaji wazi Daftari la awali la wapiga kura. Akizungumza na Viongozi hao leo ofisini kwake amewaomba Viongozi hao kwenda kuhamasisha na kutoa Elimu kwa wananchi, wafuasi wa vyama vyao ilii wajitokeze Kwa wingi katika uboreshaji Daftari Awamu ya Pili na kukagua Daftari la awali ambalo litabandikwa kwa kila kituo kilichotumika kuandikisha Wapiga kura Mwaka jana. Kwa Upande wa Viongozi wa vyama wameshukuru ushirikishwaji huo na kuhaidi kwenda kuhamasisha na kutoa Elimu kwa wananchi. Uboreshaji Daftari la Awali la Wapiga kura Jimbo la Babati Vijiji utaanza tarehe 16 Hadi tarehe 22/5 /2025, jumla ya Vituo 36 vitatumika na utafanyika ngazi ya Kata. Vituo vitafunguliwa saa 2.00 na kufungwa saa 12 jioni Kwa muda wa Siku zote Saba.
Halmashauri ya wilaya ya Babati
Anwani: P.O BOX 400, Babati.
Simu ya mezani: Simu Na. 027-2531011
Simu ya Kiganjani: 0620444641,075486577
Barua pepe: info@babatidc.go.tz,ded@babatidc.go.tz
Copyright ©2020 Babati District Council . All rights reserved.