Mashindano ya UMISSETA kitaifa yaliyokuwa yakifanyika Butimba Jijini Mwanza yamemalika ambapo Mkoa wa Manyara umeshika nafasi ya Kwanza kwenye Mchezo wa Riadha nafasi ya Pili ushangiliaji na nidhamu na kubahatikana kushika nafasi ya Nne Mshindi wa Jumla Kitaifa. Dar imeshika nafasi ya kwanza, nafasi ya Pili Mwanza, Tatu Pwani, Nne Manyara Tano Singida. Katika Mashindano hayo wasichana wawili Kutoka Mkoa wa Manyara wamechaguliwa kushiriki Mashindno ya Riadha Kitaifa ambao ni Yusta Ninga(Babati H/W Gidas S/S) na Paskalina Alex ( Mbulu Mji) .Katika Mashindano hayo Mtoto Hajara Ally kutoka H/W Babati S/S Ayatsea) amepewa tuzo ya heshima kwa kuruka juu, kujituma na juhudi binafsi.
(Picha na Habari Imeandaliwa na Afisa Habari H/W Babati)
Halmashauri ya wilaya ya Babati
Anwani: P.O BOX 400, Babati.
Simu ya mezani: Simu Na. 027-2531011
Simu ya Kiganjani: 0620444641,075486577
Barua pepe: info@babatidc.go.tz,ded@babatidc.go.tz
Copyright ©2020 Babati District Council . All rights reserved.