Baraza la Madiwani la limeagiza Timu ya menejimenti kukagua mashine za ukusanyaji mapato mara kwa mara ili kudhibiti upoteaji wa mapato ya Halmashauri . Hayo yamesemwa na Mwenyekiti wa Baraza hilo Mhe. John Noya leo kwenye Mkutano wa kwanza wa robo ya Tatu wa kujadili Taarifa za Kata uliofanyika katika Ukumbi wa H/ wilaya ya Babati." Timu ya menejimenti kagueni posi, kila mara na kudhibiti wanaokwepa kulipa mapato ya serikali "amesisitiza kiongozi huyo. Mwenyekiti huyo ametumia mkutano huo kuwashukuru madiwani kwa usimamizi wa fedha zinazopelekwa kwenye kata zao kujenga miradi ya maendeleo. Wakati huo huo Katibu Tawala Wilaya ya Babati Halfan Matipula amesisitiza madiwani kwenda maeneo yao kusikiliza na kutatua kero za wananchi. Baraza hilo limeweka msisitizo utoaji wa chakula cha mchana kwa wanafunzi katika shule zote,Vikao vya kisheria vya vijiji na vitongoji na kuongeza nguvu za ukusanyaji mapato.
Halmashauri ya wilaya ya Babati
Anwani: P.O BOX 400, Babati.
Simu ya mezani: Simu Na. 027-2531011
Simu ya Kiganjani: 0620444641,075486577
Barua pepe: info@babatidc.go.tz,ded@babatidc.go.tz
Copyright ©2020 Babati District Council . All rights reserved.