Uongozi wa H/Wilaya ya Babati leo wametembelea Vitongoji vya Kwankwari, na Bashnet kati katika Kijiji Cha Gabadaw Kata ya Nar Tarafa ya Bashnet na kutoa pole kwa Wananchi na taasisi walipatwa na madhara ya nyumba zao kuezuliwa na upepo Jana alasiri. Wakiongea na Wananchi wa Vitongoji hivyo M/kiti wa H/ Wilaya ya Babati John Noya amewapa pole Wananchi na taasisi walipatwa na matatizo hayo na amewashukuru Wananchi wengine waliojitokeza kuwasaidia" Sisi tunawapa pole waathirika wote lakini tunawashukuru Wananchi wote mliojitokeza kuchanga kuwasaidia Wananchi hao" Upepo huo umesababisha nyumba 6 za Wananchi na majengo mawili ya Hospitali ya BUMA kuezuliwa.H/Wilaya ya Babati imetoa Tsh 2 million mbili kusaidia walipatwa na majanga hayo ambapo Tsh 1 million moja itasaidia Wananchi na Tsh million moja 1 itasaidia Hospitali ya BUMA.Mbunge wa Jimbo la Babati Vijijini Mhe. Daniel Sillo ametoa bati 85Aidha Viongozi hao leo wamefanya harambee ambapo kiasi Cha Tsh 1,548,500 zimepatikana na michango inaendelea.
Halmashauri ya wilaya ya Babati
Anwani: P.O BOX 400, Babati.
Simu ya mezani: Simu Na. 027-2531011
Simu ya Kiganjani: 0620444641,075486577
Barua pepe: info@babatidc.go.tz,ded@babatidc.go.tz
Copyright ©2020 Babati District Council . All rights reserved.