Madiwani wa H/ Wilaya ya Babati Mkoani Manyara wamesisitiza vituo vya Afya vyote vilivyopokea fedha kutoka Serikali kuu kuhakikisha vinakamilika kwa wakati na kuanza kutoa huduma. Hayo yamesemwa na Mwenyekiti wa Baraza la Madiwani Mhe John Noya leo kwenye ziara ya ukaguzi miradi Kamati ya fedha uongozi na mipango ."Ukaguzi huu ni kuhakiksha miradi yote ya Vituo vya Afya vilivyopokea fedha vinakamilika ndani ya muda na kwa ubora unaotakiwa" amesisitiza Kiongozi huyo.
Katika ukaguzi wa miradi hiyo pia viongozi hao wanakutana na wananchi kuhamasisha shughuli za maendeleo ktk maeneo yao. Vituo vya Afya vilivyopokea fedha kutoka serikali kuu na vinaendelea kujengwa ni Kituo cha Afya AyasandaTsh 500Million, Kituo cha Afya Madunga Tsh 500 Millioni na Kituo cha Afya Bashnet Tsh 200 Million kutoka mapato ya ndani ya H/ Wilaya.Vituo hivyo viko hatua mbalimbali za ujenzi kama inavyoonekana kwenye picha.
Halmashauri ya wilaya ya Babati
Anwani: P.O BOX 400, Babati.
Simu ya mezani: Simu Na. 027-2531011
Simu ya Kiganjani: 0620444641,075486577
Barua pepe: info@babatidc.go.tz,ded@babatidc.go.tz
Copyright ©2020 Babati District Council . All rights reserved.