Mkuu waWilaya ya Babati. Mhe.LazaroTwange amekabidhi pikipiki 8 zilizotolewa na Serikali kwa Watendaji wa Kata 8 za pembezoni mwa H/Wilaya ya Babati kwa lengo la kuongeza ufanisi.MheTwange amekabidhi pikipiki hizo leo Ktk ofisi za Makao makuu ya H/Wilaya na kusisitiza kuwa "Mhe.Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Samia SuluhuHassan ametoa pikipiki hizi kwa ajili ya kurahisisha utendaji kazi Kwa Watendaji wa Kata,hivyo zikafanye kazi iliyokusudiwa na zitunzwe,amesisitiza kiongozi huyo.Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa H/Wilaya ya Babati Ndg.Anna Mbogo ameshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Dkt Samia Suluhu Hassan Kwa kutoa pikipiki hizo Kwa Watendaji 8 wa H/Wilaya ya Babati amesisitiza Watendaji hao kuhakikisha wanakusanya mapato ya Serikali,taarifa za mapato na Matumizi zinasomwa kwa wakati na pikipiki hizo zitunzwe. Mtendaji waKata Nkait Frank Salala kwa niaba ya Watendaji wa Kata 8 zilizopokea pikipiki ameshukuru Serikali na kuhaidi pikipiki hizo zitafanya kazi iliyokusudiwa
Halmashauri ya wilaya ya Babati
Anwani: P.O BOX 400, Babati.
Simu ya mezani: Simu Na. 027-2531011
Simu ya Kiganjani: 0620444641,075486577
Barua pepe: info@babatidc.go.tz,ded@babatidc.go.tz
Copyright ©2020 Babati District Council . All rights reserved.