Watanzania wametakiwa kuendelea kulinda amani, umoja na mshikamano uliopo ili kupata ili kujiletea maendeleo. Hayo ameyasema Katibu Tawala Wilaya ya Babati Ndg Halfan Matipula leo kwenye Mdahalo wa maadhimisho ya miaka 61 ya Uhuru wa Tanzania Bara uliofanyika katika Ukumbi wa H/ Mji wa Babati,"Sisi watanzania ni wamoja tusiwape nafasi wanaotaka kuharibu Amani ya Taifa letu" Amesisitiza kiongozi huyo" Katika Mdahalo huo wamehudhuria Viongozi na wazee Maarufu ambao walitoa mada mbalimbali za kijamii, kiuchumi na Kisiasa Mzee Jason Begashe akiwa kama mtoa mada Suala la Kijamii amesema Kuna maendeleo Makubwa yamepatika baada ya Uhuru hivyo Kila mmoja ajivunie maendeleo hayo na kutunza miradi yote inayojengwa na Serikali. Katika Mdahalo huo wamehudhuria Wakurugenzi wa taasisi na Idara za Serikali, Wakuu wa Idara na Wananchi. Aidha Timu za Mpira wa miguu, Wanafunzi wa Shule za Msingi na Sekondari walifanya vizuri kwenye uandishi wa Insha ya miaka 61 ya Uhuru walipokea vyeti na zawadi mbalimbali.
Halmashauri ya wilaya ya Babati
Anwani: P.O BOX 400, Babati.
Simu ya mezani: Simu Na. 027-2531011
Simu ya Kiganjani: 0620444641,075486577
Barua pepe: info@babatidc.go.tz,ded@babatidc.go.tz
Copyright ©2020 Babati District Council . All rights reserved.