"Tuweke masilahi yetu pembeni tuweke masilahi ya Taifa mbele,Tuanze kutengeneza ukurasa mpya Tujenge Kiru yetu"Haya ni maneno yaliyosemwa na Mkuu wa Wilaya ya Babati Mhe.Emmanuela Kaganda leo kwenye Mkutano wa kijiji cha Kiru dick kata ya Kiru H/W ya Babati wakati wa kusikiliza na kutatua kero za wananchi.Mhe.Kaganda katika mkutano amesisitiza wananchi wanaovamia shamba la Amir Estate lililoko katika kijiji hicho kuacha mara moja na kuwaeleza kuwa nchi inahitaji wawekezaji kwa ajili ya maendeleo.Wakati huohuo Mhe . Kaganda amesisitiza wananchi kuishi kwa upendo amani na ushirikiano baina yao na wawekezaji ili kujiletea maendeleo naTaifa kwa ujumla.Aidha Mhe kaganda amewaelekeza wananchi waliovunja daraja,kuvamia mashamba ya wawekezaji, wezi wajisalimishe ofisi kwake kabla hatua kali hazijachukuliwa. Katika Mkutano huo wananchi wameomba msamaha kwani yaliyokuwa yakitendeka dhidi ya uvamizi wa shamba la Amir Estate walikuwa hawana uwelewa,hii ni baada ya mkuu wa Wilaya kusoma barua zote kutoka serikali kuu.
Halmashauri ya wilaya ya Babati
Anwani: P.O BOX 400, Babati.
Simu ya mezani: Simu Na. 027-2531011
Simu ya Kiganjani: 0620444641,075486577
Barua pepe: info@babatidc.go.tz,ded@babatidc.go.tz
Copyright ©2020 Babati District Council . All rights reserved.