Walimu, Wanafunzi na Wadau wengine wa michezo katika H/ Wilaya ya Babati wameshukuru Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania( TFF) kwa kutoa mipira 160 kwa shule za msingi nne kwa ajili ya kuendeleza michezo. Hayo wameyasema leo mbele ya Mgeni Rasmi ambaye ni Mkurugenzi Mtendaji wa H/Wilaya ya Babati Anna Mbogo wakati wa hafla fupi ya ugawaji wa mpira 160 iliyofanyika katika Shule ya Msingi Dareda Kati iliyoko kata ya Ayalagaya . Naye Mkurugenzi Mtendaji Anna Mbogo kabla ya kugawa mipira hiyo ameshukuru TFF na FIFA kwa kutoa mipira hiyo katika Halmashauri ya Wilaya ya Babati na kusisitiza mipira hiyo itunzwe na ifanye kazi iliyokusudiwa ya kuchochea na kuendeleza michezo Katika Halmashauri ya Babati. Kwa upande wake Mwalimu Mkuu wa Shule ya Msingi Dareda kati Samwel Sangwa kwa niaba ya walimu shule nne zilizopokea Mipira hiyo ameshukuru TFF na FIFA kwa kutoa mipira katika shule hiyo na kuomba zoezi hilo liendelee kwa shule nyingine. Shule za msingi zilizopokea Mipira ni Shule ya Msingi Dareda Kati mipira 40,Shule ya Msingi Bashnet mipira 40, Shule ya Msingi Migungani 40 shule ya Msingi Gichameda mipira 40.
Halmashauri ya wilaya ya Babati
Anwani: P.O BOX 400, Babati.
Simu ya mezani: Simu Na. 027-2531011
Simu ya Kiganjani: 0620444641,075486577
Barua pepe: info@babatidc.go.tz,ded@babatidc.go.tz
Copyright ©2020 Babati District Council . All rights reserved.