Baraza la Madiwani la Halmashauri ya Wilaya ya Babati limeomba shirika la Umeme la TANESCO mkoa wa Manyara kupeleka umeme katika taasisi zote za H/ Wilaya ya Babati. Hayo yamesemwa leo kwenye Mkutano wa Baraza la Madiwani na Mwenyekiti wa Baraza hilo Mhe. John Noya baada ya kaimu muhandisi wa Mipango TANESCO mkoa wa Manyara Ndg Manumbo Sabi kuwasilisha taarifa kwenye Baraza hilo, "Inasikitisha shule za msingi na sekondari na baadhi ni za Bweni hazina umeme, Madiwani wakifuatilia TANESCO hawapewi majibu ya kuridhisha" amesisitiza kiongozi huyo. Mhe. Noya ameongeza Umeme kwa baadhi ya vijiji na Vitongoji ni changamoto lakini tunaomba shule zipewe kipaumbele na kupelekewa umeme haraka.Naye Muhandisi Sabi ameomba Halmashauri ya Wilaya ya Babati ipeleke orodha ya shule zote ambazo hazina umeme katika shiriki hilo ili zifanyiwe kazi.
Halmashauri ya wilaya ya Babati
Anwani: P.O BOX 400, Babati.
Simu ya mezani: Simu Na. 027-2531011
Simu ya Kiganjani: 0620444641,075486577
Barua pepe: info@babatidc.go.tz,ded@babatidc.go.tz
Copyright ©2020 Babati District Council . All rights reserved.