Baraza la Madiwani Halmashauri ya Wilaya ya Babati limesisitiza Taasisi zote zinazotoa huduma za Afya kuzingatia Taaluma na maadili ya kazi zao katika kuwahudumia wananchi. Hayo yamesemwa leo na Mwenyekiti wa Baraza hilo Mhe. John Noya kwenye mkutano wa kwanza wa Baraza hilo la kujadili taarifa za kata uliofanyika katika Ukumbi wa Halmashauri. Aidha Baraza limeshauri Kituo cha Afya Bashnet (BUMA) kinachomilikiwa na Kanisa Katoliki la Mbulu kuweka gharama za matibabu rafiki na kuzingatia maadili katika kuwahudumia wananchi. Wakati huo huo Baraza la Madiwani limewapongeza Maofisa Elimu Kata katika kusimamia Elimu katika maeneo yao na kusisitiza maofisa hao kwenda kufuatilia wanafunzi wa kidato cha kwanza ambao bado hawajaripoti shuleni na kuhakikisha wanakwenda shule kabla ya tarehe 15/2/2025
Halmashauri ya wilaya ya Babati
Anwani: P.O BOX 400, Babati.
Simu ya mezani: Simu Na. 027-2531011
Simu ya Kiganjani: 0620444641,075486577
Barua pepe: info@babatidc.go.tz,ded@babatidc.go.tz
Copyright ©2020 Babati District Council . All rights reserved.