Mkuu wa Wilaya Babati Mhe. Lazaro Twange amesisitiza utunzaji wa miundombinu yote kwenye Soko la mazao na Mbogamboga la kijiji cha Vilima vitatu kata ya Nkait H/ Wilaya ya Babati. Mhe Twange ameyasema hayo leo kijijini Vilima vitatu wakati wa kuweka jiwe la ufunguzi wa Soko hilo "Nawapongeza Halmashauri ya Wilaya ya Babati na uongozi wa kijiji cha Vilima vitatu kwa ujenzi bora wa soko hili, msisitizo ni kulitunza soko hili na kufanya usafi kila mara. Naye Mkurugenzi Mtendaji wa H/ Wilaya ya Babati Anna Mbogo amemueleza Mkuu wa Wilaya kuwa soko hilo lilikuwa kwenye hoja za Mdhibiti na Mkaguzi wa fedha za serikali yapata miaka 10 hivyo anafurahi kuona soko hilo limekamilika linatumika na hoja imefutwa kwa vitendo. Wananchi walioshiriki hafla hiyo wamefurahi wakisema wanashukuru Serikali ya Rais Samia kwa ujenzi wa soko hilo.Ujenzi Soko la vilima vitatu na choo limegharimu kiasi cha Tsh . 126,949,500/ Mpaka kukamilika kwake na linatumika.
Halmashauri ya wilaya ya Babati
Anwani: P.O BOX 400, Babati.
Simu ya mezani: Simu Na. 027-2531011
Simu ya Kiganjani: 0620444641,075486577
Barua pepe: info@babatidc.go.tz,ded@babatidc.go.tz
Copyright ©2020 Babati District Council . All rights reserved.