Uongozi wa Halmashauri ya Wilaya ya Babati mkoani Manyara umeshukuru wadau wa Maendeleo shirika la Chair the Love la nchini Marekani na Chemchem Lodge la hapa Babati kwa kutoa viti mwendo 101 kwa watu wenye mahitaji Maalum. Akitoa shukurani hizo leo katika viwanja vya Halmashauri ya Wilaya ya Babati, Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Babati Mhe. John Noya "amesema Mwaka 2024 walitukabidhi viti mwendo 70 na Mwaka huu tena wamekabidhi viti mwendo 101 Tunawashukuru Sana na ushirikiano huo uendelee".Naye Mkurugenzi wa Shirika la Chair the Love Ndg Gren Matber amesema wenyewe wameleta upendo kwa watu wenye mahitaji na kusisitiza viti hivyo wavitunze.Wakati huo huo Kaimu Mkurugenzi Mtendaji H/ ya Wilaya ya Babati Ndg Godfrey Jafary ameshukuru wadau hao na akawaomba wasichoke kuendendelea kutoa msaada kwa watu wenye Mahitaji Maalum kwani bado mahitaji ni mengi. Hafla ya upokeaji na ugawaji viti mwendo kwa watu wenye mahitaji maalum imehudhuliwa na madiwani, Watumishi na wananchi ambao kwa ujumla wao wameshukuru na kupongeza jitihada za mashirika hayo
Halmashauri ya wilaya ya Babati
Anwani: P.O BOX 400, Babati.
Simu ya mezani: Simu Na. 027-2531011
Simu ya Kiganjani: 0620444641,075486577
Barua pepe: info@babatidc.go.tz,ded@babatidc.go.tz
Copyright ©2020 Babati District Council . All rights reserved.