Serikali kwa kushirikiana na shirika lisilo la kiserikali la Karimu Heart and Spirit Organization (KAHESO) na Wananchi wa kata ya Ayalagaya wamejenga Bweni la Kisasa la Wanafunzi wenye Mahitaji maalum. Afisa Elimu Shule za Msingi H/Wilaya ya Babati Getrude Kavishe akiwa na ugeni wa Shirika hilo leo kwenye Bweni hilo lililoko shule ya Msingi Dareda kati kata ya Ayalagaya ameeleza kuwa wafadhili wametembelea bweni hilo na kuona ujenzi unavyoendelea na wamepongeza sana. Aidha Afisa Elimu amesema ujenzi huo ukikamilika utasaidia kuinua kiwango cha elimu kwa watoto wenye mahitaji maalumu wa Halmashauri ya Wilaya ya Babati na mikoa jirani kwani bweni hilo litawekwa miundombinu yote inayohitajika kwa watoto wenye mahitaji maalum. Kwa sasa bweni hilo limefikia hatua ya ukamilishaji.
Halmashauri ya wilaya ya Babati
Anwani: P.O BOX 400, Babati.
Simu ya mezani: Simu Na. 027-2531011
Simu ya Kiganjani: 0620444641,075486577
Barua pepe: info@babatidc.go.tz,ded@babatidc.go.tz
Copyright ©2020 Babati District Council . All rights reserved.