Mkuu wa Mkoa wa Manyara Mhe Queen Sendiga amepongeza Halmashauri ya Wilaya ya Babati kwa kupata Hati safi kwa Mwaka fedha 2023/ 2024 . Mhe Sendiga ameyasema hayo leo kwenye Mkutano Maalum wa Baraza la Madiwani wa kupitia hoja za Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu Hesabu za Serikali ( CAG) uliofanyika leo katika Ukumbi wa Halmashauri ya Wilaya ya Babati " Uongozi wote wa Halmashauri ya Wilaya ya Babati nawapongeza sana Kwa kupata Hati safi mfululizo kwa miaka mitatu" amesisitiza kiongozi huyo. Wakati huo huo Mhe. Sendiga ameagiza wakuu wa Idara Kila mmoja kuzuia hoja katika Idara zake . Kwa Upande wake Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Babati Mhe. John Noya ameshukuru Mkuu wa Mkoa kwa kazi nzuri ya kuhakikisha kila Halmashauri inaendeshwa kwa kuzingatia Sheria kanuni na taratibu Ili kuwaletea wananchi maendeleo .
Halmashauri ya wilaya ya Babati
Anwani: P.O BOX 400, Babati.
Simu ya mezani: Simu Na. 027-2531011
Simu ya Kiganjani: 0620444641,075486577
Barua pepe: info@babatidc.go.tz,ded@babatidc.go.tz
Copyright ©2020 Babati District Council . All rights reserved.