Mkuu wa Mkoa wa Manyara Mhe. Joseph Joseph Mkirikiti amezipongeza Kaya zilizoko kwenye Mpango wa kunusuru Kaya Masikini TASAF zinazopokea fedha na kuzitumia vizuri katika shughuli za Maendeleo. Hayo amesema leo kwenye Mkutano wa hadhara Kijiji cha Matufa Kata ya Magugu H/Wilaya ya Babati. " Ni wapongeze sana kaya zote zinazopokea fedha za Mpango wa Kunusuru Kaya Masikini TASAF kwa kufanya shughuli za maendeleo ktk maeneo yenu" amesisitiza kiongozi huyo. Aidha Katika mkutano huo Mkuu wa Mkoa wa Manyara ameagiza Serikali ya Kijiji cha Matufa kuhakikisha Watoto wote wa Shule ya Msingi wanapata chakula cha mchana shuleni. "Kaeni na Wazazi mjipange, watoto wapate chakula shuleni na wazazi àmbao hawapeleki chakula wachukuliwe hatua za kisheria". amesisitiza Mkuu wa Mkoa.Katika Mkutano huo Mkuu wa Mkoa amesikiliza kero za Wananchi na kuzitatua kisha akatembelea Wanufaika wa Mpango wa Kunusuru kaya Masikini TASAF na kuona walivyonufaika na Mpango huo.
Halmashauri ya wilaya ya Babati
Anwani: P.O BOX 400, Babati.
Simu ya mezani: Simu Na. 027-2531011
Simu ya Kiganjani: 0620444641,075486577
Barua pepe: info@babatidc.go.tz,ded@babatidc.go.tz
Copyright ©2020 Babati District Council . All rights reserved.