Mkuu wa Mkoa wa Manyara Mhe Queen Sendiga ameagiza Halmashauri zote za Mkoa wa Manyara kuhakikisha fedha zote zinakusanywa, kusimamiwa na kutumika vizuri katika shughuli za maendeleo. Mhe. Sendiga ameyasema hayo leo Halmashauri ya wilaya ya Babati kwenye kikao kazi cha madiwani na timu ya menejimenti " fedha yote iliyokisiwa ikusanywe,itumike vizuri kwenye miradi ya maendeleo" amesisitiza kiongozi huyo. Wakati huo huo ameagiza Wahandisi na Maofisa ugavi wote Mkoa wa Manyara, kusimamia miradi, kwa uadilifu, ubora na haki ili fedha zote zinazotolewa zikamilishe miradi yote na kwa wakati. Naye Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Babati Mhe. John Noya amemueleza Mkuu wa Mkoa kuwa Halmashauri inaendelea na ukusanyaji wa Mapato mpaka sasa imefika asilimia 57 na inaendelea kutenga fedha na kupeleka asilimia 40 kila mwezi kwenye miradi ya maendeleo.
Halmashauri ya wilaya ya Babati
Anwani: P.O BOX 400, Babati.
Simu ya mezani: Simu Na. 027-2531011
Simu ya Kiganjani: 0620444641,075486577
Barua pepe: info@babatidc.go.tz,ded@babatidc.go.tz
Copyright ©2020 Babati District Council . All rights reserved.