Baraza la Madiwani la H/Wilaya ya Babati limejadili na kupitisha rasimu ya Sheria ndogo ya kuzuia na kudhibiti sumukuvu za mwaka 2022.Akizungumza kwenye Mkutano wa Baraza hilo uliofanyika leo kwenye Ukumbi wa H/ Wilaya Mwenyekiti wa Baraza hilo Mhe.John Noya amesema lengo la kutunga Sheria hiyo ni kuzuia kuenea kwa sumu kuvu ambayo inamadhara makubwa kwa Jamii na kiuchumi naye Mkurugenzi Mtendaji wa H/Wilaya Ndg Anna Mbogo amesema kupitishwa Kwa rasimu hiyo kutasaidia wadau wote wanaohusika na kilimo,biashara na usafirishaji wa mazao kuhakikisha mazao yao yavunwa,kutunzwa na kusafirishwa Ktk mazingira salama ili mtumiaji asipate magonjwa yatokanayo na sumukuvu.
Kabla ya Mkutano wa Baraza kuanza Afisa Kilimo Leornad Masesa ametoa mafunzo juu ya Sumukuvu,madhara na namna ya kudhibiti sumu hiyo.Madiwani wote wamekubaliana kwenda kutoa Elimu ya Sumukuvu kuanzia ngazi ya Vitongoji na vijiji ili Wananchi wajue ukweli kuhusu Sumukuvu.Naye Mwanasheria wa H/ Wilaya Godfrey Balaza amesema Elimu ya Sumukuvu niendelevu.
Halmashauri ya wilaya ya Babati
Anwani: P.O BOX 400, Babati.
Simu ya mezani: Simu Na. 027-2531011
Simu ya Kiganjani: 0620444641,075486577
Barua pepe: info@babatidc.go.tz,ded@babatidc.go.tz
Copyright ©2020 Babati District Council . All rights reserved.