Mwenyekiti wa H/Wilaya ya Babati Mhe . John Noya leo amemkabidhi Mkuu Wilaya ya Babati Mhe. Lazaro Twange madarasa 89 ambapo sekondari ni madarasa 78 na shule Shikizi ni madarsa 11 yenye gharama ya Tsh 1,650,068,833 yaliokamilika kwa asilimia 100 yaliotekelezwa na Mpango wa Maendeleo kwa ustawi wa Taifa na Mapambano dhidi ya UVIKO -19 katika sekta ya Elimu H/ Wilaya ya Babati. Akipokea Madarasa hayo kwenye Hafla fupi iliyofanyika katika shule ya Msingi Kazaroho iliyoko kijiji cha Kazaroho Kata ya Kisangaji, Mkuu wa Wilaya ya Babati Mhe. Twange amemshukuru Mhe. Rais kwa kutoa fedha hizo kwa ajili ya ujenzi wa madarasa na kumuomba Mhe. Rais kuendelea kutoa fedha kwa Wilaya ya Babati ili kutekeleza miradi ya Maendeleo.Aidha Mkuu wa Wilaya ya Babati amewashukuru viongozi wa H/Wilaya ya Babati,wakuu wa Idara Madiwani ,watendaji, Wakuu wa shule , viongozi na wananchi kuanzia ngazi ya kitongoji kwa ushirikiano na kufanya kazi kwa bidii mpaka ujenzi wa madarasa hayo kukamilika kwa wakati
Halmashauri ya wilaya ya Babati
Anwani: P.O BOX 400, Babati.
Simu ya mezani: Simu Na. 027-2531011
Simu ya Kiganjani: 0620444641,075486577
Barua pepe: info@babatidc.go.tz,ded@babatidc.go.tz
Copyright ©2020 Babati District Council . All rights reserved.