Mwanariadha wa Kimataifa mzawa wa Mkoa wa Manyara kutoka kata ya Madunga Wilayani Babati Gabriel Gerald Geay leo Mei 28 mwaka 2025 ametembelea kambi ya UMITASHUMTA ya Halmashauri ya Wilaya ya Babati, kwa kutoa msaada wa Track suit na kuahidi zawadi nyingi kwa vijana wa riadha watakaopata medali ama kuchaguliwa kuendelea na michezo kwenye timu ya Mkoa, amekabidhi zawadi hizo kwa Afisa Elimu msingi wa Halmashauri ya Wilaya hiyo mwalimu Getrude Kavishe, Michezo hiyo, inafanyika katika shule ya msingi Dareda Kati ambapo timu inajiandaa kwenda ngazi ya mkoa na hatimaye Mkoani Iringa ambapo mashindano yatafanyika kitaifa.
Halmashauri ya wilaya ya Babati
Anwani: P.O BOX 400, Babati.
Simu ya mezani: Simu Na. 027-2531011
Simu ya Kiganjani: 0620444641,075486577
Barua pepe: info@babatidc.go.tz,ded@babatidc.go.tz
Copyright ©2020 Babati District Council . All rights reserved.