Katika kipindi hiki cha Mwezi August na Septamba ni kipindi cha Kiangazi kwa mkoa wa Manyara, lakini Wananchi wa Kata ya Madunga Tarafa ya Bashnet H/Wilaya ya Babati kwao ni neema kama unavyoona kwenye picha. Wananchi wanatumia kipindi hiki kulima vitunguu saumu na vitunguu maji kwa wingi ili kujipatia kipato.Mtendaji wa Kijiji cha Utwali Syilvester Opapa anasema Bonde la mto Endayaya ni chanzo cha Mapato kwa wananchi wa Kata hiyo kwani hutumika kwa kilimo mwaka mzima kwa kulima mazao mbalimbali na kuna kilimo cha umwagiliaji ambacho chanzo cha Maji hayo ni msitu wa Nou . Mtendaji huyo ameomba wananchi wa Kata za Madunga na Qameyu kuendelea kutunza mazingira ili bonde hilo liwanufaishe wananchi na taifa kwa ujumla.Bonde hilo hulimwa mahindi, vitunguu, viazi na mazao mengine kwa mwaka mzima.
Halmashauri ya wilaya ya Babati
Anwani: P.O BOX 400, Babati.
Simu ya mezani: Simu Na. 027-2531011
Simu ya Kiganjani: 0620444641,075486577
Barua pepe: info@babatidc.go.tz,ded@babatidc.go.tz
Copyright ©2020 Babati District Council . All rights reserved.