Mradi wa kufungua barabara za vitongoji wapongezwa na wananchi Halmashauri ya Wilaya ya Babati mkoani Manyara.Mradi huu unatekelezwa na Walengwa waTASAF kupitia ajira za muda .Wakizungumza leo kwa nyakati tofauti wananchi wa Vijiji vya Kwaraa, Endanachan, Ayamango, Qameyu waliokutwa wakitengeneza barabara hizo za vitongoji wamesema kupitia mradi huu wameweza kufungua barabara zinazounganisha vijiji na vitongoji na vitongoji kwa vitongoji.Wananchi hao wameeleza kuwa barabara zilizofunguliwa zitasaidia kupitika kwa urahisi,kusafirisha mazao yao kutoka shambani kwenda sokoni na kuunganisha vijiji na vitongoji kwenye mawasiliano ya mtandao wa barabara.Jumla ya vijiji 102 vya H/ Wilaya ya Babati vinatekeleza mradi wa ufunguzi wa barabara za Vitongoji kupitia ajira za muda unaotekelezwa na Walengwa wa TASAF.
Halmashauri ya wilaya ya Babati
Anwani: P.O BOX 400, Babati.
Simu ya mezani: Simu Na. 027-2531011
Simu ya Kiganjani: 0620444641,075486577
Barua pepe: info@babatidc.go.tz,ded@babatidc.go.tz
Copyright ©2020 Babati District Council . All rights reserved.