Halmashauri ya Wilaya ya Babati imeanzisha Mnada mwingine katika kijiji cha Gabadaw kata ya Nar. Mwenyekiti wa Baraza la Madiwani wa H/ Wilaya Babati Mhe John Noya ameeleza Mkutano wa Baraza la Madiwani leo unaofanyika katika ukumbi H/ Wilaya ya Babati kuwa Halmashauri yetu imeanzisha mnada mpya wa Gabadaw ulioko katika kijiji cha Gabadaw utakaokuwa unafanyika kila tarehe 22 ya kila mwezi. " Nitumie mkutano huu wa kujadili mpango na bajeti wa mwaka 2024/2025 kuwatangazia madiwani na wananchi wote kuwa tumeanzisha mnada mpya utakaofanyika kijiji cha Gabadaw kata ya Narr kila tarehe 22 ya mwezi nia ni kuongeza mapato ya Halmashauri "Amesisitiza kiongozi huyo . Aidha ametumia fursa hiyo kuwaalika wananchi na viongozi mbalimbali kupeleka bidhaa na huduma katika mnada huo.
Halmashauri ya wilaya ya Babati
Anwani: P.O BOX 400, Babati.
Simu ya mezani: Simu Na. 027-2531011
Simu ya Kiganjani: 0620444641,075486577
Barua pepe: info@babatidc.go.tz,ded@babatidc.go.tz
Copyright ©2020 Babati District Council . All rights reserved.