Mkuu wa Wilaya ya Babati Mhe. Eng. Raymond Mushi amewata wananchi kulinda amani katika maeneo yote ya Vijiji na Vitongoji ili kujiletea maendeleo. Hayo amesema Katika Kijiji cha Luxmanda Kata ya Secheda Tarafa ya Bashnet wakati akifunga mafunzo ya Jeshi la Akiba katika Kata ya Secheda. "Haiwezekani tukawa na jeshi la Akiba ,Ukosefu wa Amani na Gongo Vikasumbua" Hivyo nendeni mkalinde amani na kuzuia Gongo katika vitongoji na vijiji Mkuu wa Wilaya alisisitiza. Aidha ameagiza jeshi hilo kwenda kusaka gongo katika vijiji vyote ndani Kata ya Secheda na kuimaliza kwa muda wa siku saba (7) kisha kuhamia Kata ya Nar. Aidha Mkuu wa Wilaya aliwashukuru vijana waliomaliza mafunzo hayo na kuwashukuru wananchi, na wadau mbalimbali waliowezesha kufanyika mafunzo hayo. Akisoma Risala ya wahitimu hao Ndg Juma Tlatla, alisema Vijana waliojiandikisha kuanza mafunzo hayo ni 880 na waliobahatika kumaliza ni vijana 117 na wanaomba kupewa kipaumbele nafasi za JKTzinazojitokeza ambapo Mkuu wa Wilaya alikubali pendekezo hilo.
Halmashauri ya wilaya ya Babati
Anwani: P.O BOX 400, Babati.
Simu ya mezani: Simu Na. 027-2531011
Simu ya Kiganjani: 0620444641,075486577
Barua pepe: info@babatidc.go.tz,ded@babatidc.go.tz
Copyright ©2020 Babati District Council . All rights reserved.