Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Babati Anna Mbogo amepongeza mtandao wa vikundi vya Tembo pilipili kwa uhifadhi rafiki wa wanyamapori na mazingira. Hayo ameyasema leo kwenye Kongamano la Vikundi vya kukabiliana na Tembo kwa njia rafiki lililofanyika katika kijiji cha Moyamayoka kata ya Mwada "Kongamano hili pamoja na mafunzo tuliopata limetupa njia rafiki yakukabiliana na Tembo kuharibu mazao na kuvamia makazi ya watu iitwayo Chill fance twende tukazitumie na kuwafundisha wengine katika maeneo yetu" amesisitiza kiongozi huyo. Aidha amepongeza wadau wote walioshiriki kuandaa kongamano na kutoa mafunzo katika vikundi hivyo kuwa njia hiyo itasaidia kupunguza hadha ya tembo kuharibu mazao na kuvamia makazi. Vikundi vilivyo shiriki kongamano hilo ni tembo pilipili Tarangile, Lake Manyara na Ngorongoro .
Halmashauri ya wilaya ya Babati
Anwani: P.O BOX 400, Babati.
Simu ya mezani: Simu Na. 027-2531011
Simu ya Kiganjani: 0620444641,075486577
Barua pepe: info@babatidc.go.tz,ded@babatidc.go.tz
Copyright ©2020 Babati District Council . All rights reserved.