Katika utamaduni wa Mtanzania, ukifanya vizuri utapewa zawadi, Hii imeshangaza na kuvutia wengi kuona wahe. Madiwani wa Halmashauri wa Wilaya ya Babati Mkoani Manyara wakitoa pongezi na zawadi nyingi kwa Mkurugenzi Mtendaji Anna Mbogo.Wakiongea katika Mkutano Maalum wa Baraza la Madiwani wa kuvunja Baraza hilo leo katika Ukumbi wa Halmashauri, Madiwani hao wamesema wametoa zawadi na pongezi kwa Mkurugenzi Mtendaji huyo kwa kuthamini uongozi wake , ujenzi wa miradi mikubwa, ufuatiliaji wa miradi, msikivu na mtu anaye jali watu wote. Siku ya kuvunja Baraza la Madiwani limetanguliwa na Dua ya kuliombea Taifa na Halmashauri na kusoma taarifa ya mafanikio katika sekta zote kwa kipindi cha Mwaka 2020 hadi 2025.ili Somwa na Mkurugenzi huyo na kuonesha mafanikio Kwa Kila kata.
Halmashauri ya wilaya ya Babati
Anwani: P.O BOX 400, Babati.
Simu ya mezani: Simu Na. 027-2531011
Simu ya Kiganjani: 0620444641,075486577
Barua pepe: info@babatidc.go.tz,ded@babatidc.go.tz
Copyright ©2020 Babati District Council . All rights reserved.