Mkuu wa Mkoa wa Manyara Mhe. Joseph Mkirikiti ameitaka jamii na wanafunzi kuheshimu na kuitunza miundombinu ya shule inayojengwa na Serikali na jamii kwa ujumla ili ilete maendeleo endelevu. Kiongozi huyo ameyasema leo kwenye hafla fupi ya Makabidhiano ya Bati 950 kutoka Bank ya NMB iliyofanyika ktk shule ya Sekondari Gallapo Kata na Kijiji cha Gallapo H/Wilaya ya Babati, "Tunawashukuru sana Bank ya NMB kwa mchango wa Bati 950 yenye thamani ya Tsh 28,180,000 kwa H/ W ya Babati tunasema umepunguza kazi kwa Wazazi na Serikali" amesisitiza kiongozi huyo. Awali Mkurugenzi Mtendaji wa H/Wilaya ya Babati Ndg John J. Nchimbi amemshukuru Meneja wa NMB Kanda ya Kati Ndg Msolo Mlonzi kwa msaada huo na kusema utapunguza vyuma vya madarasa yaliyokuwa yanahitajika kwa ajili ya Wanafunzi wa kidato cha kwanza mwaka 2021.
Halmashauri ya wilaya ya Babati
Anwani: P.O BOX 400, Babati.
Simu ya mezani: Simu Na. 027-2531011
Simu ya Kiganjani: 0620444641,075486577
Barua pepe: info@babatidc.go.tz,ded@babatidc.go.tz
Copyright ©2020 Babati District Council . All rights reserved.