Mwenge wa uhuru umepokelewa katika Kijiji cha Magara kata ya Magara H/Wilaya Babati leo Julai 15, 2024 ambapo umekimbizwa kilomita 120 pamoja na kufungua, kutembelea na kuzindua na kuona miradi 7 yenye jumla ya thamani ya Tsh Bilioni 71.2 kwa Halmashauri ya Wilaya ya Babati.Mwenge wa Uhuru umekesha viwanja vya stendi kata ya Magara ambapo kongamano la vijana, maonesho shughuli mbalimbali za Lishe, madawa ya kulevya, malaria uchaguzi, na utunzaji wa mazingira na uchanguzi zimefanyika.Miradi ya Ujenzi wa Maabara shule ya sekondari Tara Getty, Mradi wa maji magara, mradi wa ujenzi wa wa box culvat, kuona ujasirimali kwa kikundi cha Vijana Magugu Rice,Ujenzi wa Zahanati ya Ngoley kiwanda kutengeneza Mbolea Phosphate Intracom vilima vitatu mradi wa utunzaji na ufugaji nyuki vilipitiwa na mbio za mwenge."Tunza Mazingira na Shiriki Uchaguzi wa Serikali za Mitaa kwa Ujenzi wa Taifa Endelevu"
Halmashauri ya wilaya ya Babati
Anwani: P.O BOX 400, Babati.
Simu ya mezani: Simu Na. 027-2531011
Simu ya Kiganjani: 0620444641,075486577
Barua pepe: info@babatidc.go.tz,ded@babatidc.go.tz
Copyright ©2020 Babati District Council . All rights reserved.