Mkuu wa Wilaya ya Babati Mhe. Elizabeth Kitundu amesitisha Michezo ya Kubahatisha kufanyika katika Halmashauri ya Wilaya ya Babati kutokana na Halmashauri hiyo kutokuwa na mahali panapokidhi kuweka mashine ya michezo ya kubahatisha.Akitoa taarifa ya Serikali leo kwenye Baraza la Madiwa la Halmashauri ya Wilaya ya Babati lililofanyika katika Makao mapya ya H/Wilaya,Mkuu waWilaya amesema kumekuwa na malalamiko mengi kutoka kwa Viongozi na wananchi juu michezo hiyo kuwekwa maeneo ya wazi kv duka au nyumba ya mtu, Vijana kutofanya kazi ,mchezo huo kufanyika muda wa kazi na watoto Wengine hawaendi shule kutokana na michezo hiyo,"Katika H/Wilaya ya Babati hakuna mahali panapokidhi kuweka michezo ya kubahatisha michezo hiyo ipelekwe sehemu za Mjini" Amesisitiza Mkuu wa Wilaya. Aidha ameagiza Mkurugenzi kusitisha kukata leseni ya michezo hiyo na Maofisa Tarafa,Watendaji wa Kata na Vijiji kusimamia agizo hilo .
Halmashauri ya wilaya ya Babati
Anwani: P.O BOX 400, Babati.
Simu ya mezani: Simu Na. 027-2531011
Simu ya Kiganjani: 0620444641,075486577
Barua pepe: info@babatidc.go.tz,ded@babatidc.go.tz
Copyright ©2020 Babati District Council . All rights reserved.