Madiwani wa Halmashauri ya Wilaya ya Babati Mkoa wa Manyara wameshukuru Serikali kwa ujenzi wa jengo la Makao Makuu. Wakiongea kabla ya kuvunja Baraza la Madiwani leo katika Ukumbi wa Halmashauri wamesema pamoja na Miradi mingi katika Kata zao Wanashukuru na kuipongeza Serikali inayoongozwa na Mhe. Dkt Samia Suluhu Hassan Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa ujenzi wa jengo zuri la kisasa la Makao Makuu ya Halmashauri ya Wilaya ya Babati. Mwenyekiti wa Baraza hilo Mhe. John Noya amesema hayo ni mafanikio makubwa wanayojivunia Madiwani na Wananchi wa H/ Wilaya ya Babati kwa Serikali ya Awamu ya Sita. Amesisitiza kiongozi huyo. Jengo zuri la Halmashauri ya Wilaya ya Babati limejengwa katika Kijiji Endasago Kata ya Arri Tarafa ya Bashnet Barabara mkuu kuelekeza Singida .
Halmashauri ya wilaya ya Babati
Anwani: P.O BOX 400, Babati.
Simu ya mezani: Simu Na. 027-2531011
Simu ya Kiganjani: 0620444641,075486577
Barua pepe: info@babatidc.go.tz,ded@babatidc.go.tz
Copyright ©2020 Babati District Council . All rights reserved.