Madiwani wa Halmashauri ya Wilaya ya Babati wametakiwa kutekeleza kwa vitendo mambo mazuri waliojifunza katika Halmashauri ya Jiji la Mwanza ili kuwaletea maendeleo Wananchi.Hayo ameyasema leo Mhe. Bhiku Kotecha Naibu Mstahiki Meya wa Jiji la Mwanza wakati wa ziara ya Mafunzo ya Wahe. Madiwani wa Halmashauri ya Wilaya ya Babati katika Jiji la Mwanza, "Mmekuja kujifunza , tumetembelea miradi yenye manufaa kwa wananchi naomba mazuri nendeni mkayatekeleze kwa vitendo amesisitiza kiongozi huyo, naye Mwenyekiti wa Halmashauri Wilaya ya Babati Mhe. John Noya amesema yote waliojifunza wanaenda kuyatekeleza mara moja. Madiwani wa H/Wilaya ya Babati wako ziara ya Mafunzo Jiji la Mwanza kujifunza mbinu bora za ukusanyaji mapato ya ndani,utekelezaji wa Miradi ya Maendeleo kupitia fedha za mapato ya ndani na uwezeshaji Wananchi kiuchumi
Halmashauri ya wilaya ya Babati
Anwani: P.O BOX 400, Babati.
Simu ya mezani: Simu Na. 027-2531011
Simu ya Kiganjani: 0620444641,075486577
Barua pepe: info@babatidc.go.tz,ded@babatidc.go.tz
Copyright ©2020 Babati District Council . All rights reserved.