Mkuu wa Wilaya ya Babati, Mhe. Emmanuela Mtatifikolo Kaganda, ameongoza kikao muhimu cha maandalizi ya mapokezi ya Mwenge wa Uhuru unaotarajiwa kukimbizwa katika Halmashauri za Wilaya ya Babati mwezi Julai, 2025.
Kikao hicho kimefanyika leo mapema katika ukumbi wa Halmashauri ya mji Wa Babati, kikihusisha wajumbe kutoka Halmashauri zote mbili (Mji na Wilaya), pamoja na wakuu wa taasisi mbalimbali, mashirika ya maendeleo na vyombo vya ulinzi na usalama vilivyopo ndani ya Wilaya pamoja na viongozi Wa Chama.
Katika kikao hicho, Mhe. Kaganda amesisitiza umuhimu wa maandalizi ya kina, ushirikiano wa wadau wote, na kuhakikisha kuwa miradi itakayopitiwa na Mwenge inazingatia ubora, thamani ya fedha na maslahi ya wananchi. Aidha, amewataka viongozi wa kata, mitaa na vijiji kushirikiana kwa karibu na kamati ya maandalizi ili kuhakikisha mapokezi hayo yanakuwa ya kibunifu, salama na yenye hamasa ya kitaifa.
Mwenge wa Uhuru utakapowasili, unatarajiwa kukimbizwa katika maeneo mbalimbali ya Wilaya, kutembelea miradi ya maendeleo, kuhamasisha mapambano dhidi ya rushwa, dawa za kulevya, UKIMWI, na kusisitiza amani kuelekea uchaguzi mkuu wa 2025.
Halmashauri ya wilaya ya Babati
Anwani: P.O BOX 400, Babati.
Simu ya mezani: Simu Na. 027-2531011
Simu ya Kiganjani: 0620444641,075486577
Barua pepe: info@babatidc.go.tz,ded@babatidc.go.tz
Copyright ©2020 Babati District Council . All rights reserved.