Mkuu wa Wilaya ya Babati Mhe. Emanuela Kaganda amesisitiza maafisa usafirishaji kufuata Sheria za barabarani ili kuepusha ajali. Mhe. Kaganda ameyasema hayo leo katika viwanja vya ofisi za mkuu wa Wilaya wakati akikabidhi pikipiki 10 kwa vikundi viwili vya vijana vya Halmashauri ya Wilaya ya Babati ." Leo tunawakabidhi pikipiki hizi hakikisha zisitumike kwenye uharifu na zitunzeni wa faida ya familia na jamii inayotuzunguka" amesisitiza kiongozi huyo..Naye Kaimu Mkurugenzi Mtendaji Godfrey Jafary amesema kwa Mwaka huu Halmashauri imetoa mkopo Kwa vikundi 46 vya Wanawake ,9 vya vijana na 3 vya watu wenye ulemavu jumla ya Tsh 452,000,000/ zimekoposhwa Kwa makundi maalum na akasisitiza vijana hao kuhakikisha wanafanya marejesho kwa wakati.Vijana waliokabidhiwa pikipiki wameshukuru Serikali ya Awamu ya Sita Kwa kutoa mikopo kwenye vikundi Ili kupata mtaji na kujiari .
Halmashauri ya wilaya ya Babati
Anwani: P.O BOX 400, Babati.
Simu ya mezani: Simu Na. 027-2531011
Simu ya Kiganjani: 0620444641,075486577
Barua pepe: info@babatidc.go.tz,ded@babatidc.go.tz
Copyright ©2020 Babati District Council . All rights reserved.