Mkuu wa Wilaya ya Babati Mhe. Lazaro Twange ameagiza kituo Cha Afya Madunga kuanza kutumika tarehe 15/11/2022. Mkuu wa Wilaya ameyasema hayo leo kwenye Mkutano wa Baraza la Madiwani la H/ Wilaya ya Babati lililofanyika leo Ktk ukumbi wa H/ Wilaya ya Babati. " Serikali imeendelea kutoa fedha nyingi zinazotekeleza miradi ya maendeleo Ktk sekta ya Afya na Elimu, hivyo miradi hiyo isimamiwe kikamilifu na ianze kutoa huduma Kwa Wananchi" amesisitiza kiongozi huyo. Aidha amesisitiza vituo vingine vya Afya vya Bashnet na Ayasanda ujenzi ukamilike ili Wananchi wapate huduma iliyokusudiwa. H/ Wilaya ya Babati inavyo vituo vitano vinavyojengwa na Serikali na ujenzi unaendelea ambavyo ni, Gidas, Ayasanda, Bashnet, Ayasanda na Madunga.
Halmashauri ya wilaya ya Babati
Anwani: P.O BOX 400, Babati.
Simu ya mezani: Simu Na. 027-2531011
Simu ya Kiganjani: 0620444641,075486577
Barua pepe: info@babatidc.go.tz,ded@babatidc.go.tz
Copyright ©2020 Babati District Council . All rights reserved.