Kituo Cha Afya Gallapo kilichopo kata ya Gallapo H/Wilaya ya Babati kimepata gari lenye Na. STL 0048 kwa ajili ya kubeba Wagonjwa ( Ambulance) . Akitoa Taarifa hiyo leo kwenye uzinduzi wa gari hili katika viwanja vya H/ Wilaya ya Babati, Mkurugenzi Mtendaji Anna Mbogo amesema "Tunashukuru Wajumbe wa Baraza la Madiwani kwa maelekezo ya kutengeneza gari hili na sasa liko tayari"; amesisitiza kiongozi huyo. . Kwa Upande wake Mwenyekiti wa H/ Wilaya ya Babati Mhe. John Noya ameshukuru Timu ya Menejimenti kwa kutengeneza gari hilo Ili kusaidia wananchi wa Kanda ya Gallapo na Tarafa ya Babati kwa ujumla. Mpaka sasa H/ Wilaya ya Babati imewezesha Vituo vya Nkait, Magugu, Bashnet, kupata magari ya Wagonjwa na sasa ni Gallapo na itaendelea kupeleka magari katika vituo vya afya vingine
Halmashauri ya wilaya ya Babati
Anwani: P.O BOX 400, Babati.
Simu ya mezani: Simu Na. 027-2531011
Simu ya Kiganjani: 0620444641,075486577
Barua pepe: info@babatidc.go.tz,ded@babatidc.go.tz
Copyright ©2020 Babati District Council . All rights reserved.