Mkuu wa Wilaya ya Babati Mhe.LazaroTwange amewataka wafanyabiashara Wilaya Babati kujiandaa vyema na kutumia fursa Kwa ajili ya kilele Cha Mbio za Mwenge wa Uhuru utakaofanyika trh14/10/2023 kitaifa Mkoa wa Manyara.Hayo ameyasema leo kwenye kikao baina yake na Chemba ya Wafanyabiashara ,Wakulima na Wenyeviwanda(TCCIA) kilichofanyika Ktk ukumbi wa H/Mji wa Babati "Mkoa wa Manyara umepewa heshima ya Kilele Cha Mbio za Mwenge wa Uhuru kitaifa,Wiki ya Vijana na Kumbukumbu ya Kifo Cha Hayati Baba wa Taifa mwaka huu, Sisi kama Wafanyabiashara,Wakulima na wazalishaji tujiandae vizuri kutumia fursa hiyo kwa ajili ya maendeleo yetu" amesisitiza kiongozi huyo.Mkuu wa Wilaya amewaomba wafanyabiashara kuanza mapema,kuwekeza na kuboresha shughuli ambazo zitawaongezea kipato na kupata faida.Aidha amewaomba wajumbe wa TCCIA kusaidia shughuli mbalimbali mara watakapojulishwa.Naye Mkiti wa TCCIA Mussa Chelema ameshukuru kwa ushirikishwaji huo na wamekubali kwenda kuhamasisha wafanyabiashara wengine kuanza maandalizi.
Halmashauri ya wilaya ya Babati
Anwani: P.O BOX 400, Babati.
Simu ya mezani: Simu Na. 027-2531011
Simu ya Kiganjani: 0620444641,075486577
Barua pepe: info@babatidc.go.tz,ded@babatidc.go.tz
Copyright ©2020 Babati District Council . All rights reserved.